Blatter: Huwezi kununua kombe la dunia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Blatter

Aliyekuwa rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter amesisitiza kuwa kura ya kuandaa kombe la dunia mwaka 2022 haikupangwa ,akisema ''huwezi kununua kombe la dunia''.

Blatter alisema kwamba hana hatia kufuatia madai ya ufisadi huku akingoja uamuzi wa rufaa yake aliyoikata dhidi ya marufuku ya miaka nane aliyopigwa na FIFA.

Nina hakika kutakuwa na uamuzi wa haki na kwamba sijafanya uhalifu wa aina yoyote. Alisema Blatter.

FIFA ltamchagua rais wake mpya mnamo tarehe 26 mwezi Februari

Blatter alishinda kiti hicho kwa mara ya tano mnamo mwezi Mei lakini akapigwa marufuku kwa miaka minane kwa kumlipa pauni milioni 1.3 rais wa UEFA aliyesimamishwa kazi Michel Platini,malipo yanayodaiwa kuwa na utata.