Barcelona:EPL ni mpinzani mkuu kuliko Real

Image caption Rais wa kilabu ya Barcelona

Ligi ya Uingereza ni mpizani mkubwa wa Barcelona ikilinganishwa na Real Madrid,amesema rais wa kilabu hiyo Josep Maria Bartomeu.

Kilabu 20 za ligi kuu ya Uingereza zitaanza kugawanya kitita cha pauni bilioni 5.136 za matangazo ya moja kwa moja kuanzia msimu ujao.

''Timu za ligi ya Uingereza zitakuwa na ubabe wa kifedha kuanzia sasa na tuna wasiwasi,''Bartomeu aliiambia BBC Sports.

Kilabu ya Barcelona inakabiliana na Arsenal katika ligi ya vilabu bingwa Ulaya siku ya Jumanne.

Image caption Wachezaji wa ligi kuu ya Uingereza

Kikosi cha Luis Enrique kitaanza awamu ya kwanza ya kombe hilo katika uwanja wa Emirates kikiwa hakijafungwa katika mechi 32 za ligi na zile za kombe la ligi hiyo huku kikitaka kushinda kombe hilo kwa msururu.

Kilabu kubwa za Uhispania -Barca na Real Madrid,zilijadili kuhusu mikataba yake ya mechi za ligi hiyo zinazoonyeshwa moja kwa moja katika runinga lakini sasa zimezuia kufanya hivyo kupitia sheria mpya ya Uhispania.