Davis cup: Murray kuiongoza uingereza

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Andy Murray kuiongoza Uingereza michuano ya Tenisi, Davis Cup

Mcheza Tenisi Andy Murray anatarajia kuiongoza Uingereza katika mchezo dhidi ya Japan mashindano ya Tenisi ya Davis Cup ikiwa ni mchezo wa raundi ya kwanza kuweza kushinda mjini Birmingham kuanzia tarehe 4-6 mwezi March.

Murray mwenye miaka 28 anayeshika namba mbili ya ubora ulimwenguni ataungana na Jamie , Kyle Edmund, Dominic Inglot pamoja na Dan Evans.

Uingereza ilishinda katika mashindano ya Davis cup kwa mara ya kwanza mwaka 1936 dhidi ya ubelgiji .