Infantinho na matumaini ya ushindi Fifa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mgombea Urais Fifa, Gianni Infantino

Mgombea urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Gianni Infantino ana uhakika kuwa atakusanya kura nyingi kutoka mataifa ya Afrika katika uchaguzi Ijumaa hii.

Infantino alifanya ziara fupi Afrika Kusini kwa mwaliko wa hasimu wake katika kinyang'anyiro hicho Tokyo Sexwale ambapo wawili hao walikutana katika kisiwa cha Robben, gereza ambalo Sexwale aliwahi kufungwa katika kipindi cha ubaguzi wa rangi.

Lakini pamoja na Shirikisho la Soka la Afrika-CAF kutoa msimamo wake kuwa watamuunga mkono Sheikh Salman bin Ibrahim al-Khalifa wa Bahrain, katibu mkuu huyo wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA amesema ana uhakika wa kuungwa mkono na mataifa ya Afrika.