Zidane:Nawahitaji Pogba, Tielemans

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane

Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane amepanga kuwawania Paul Pogba na Youri Tielemans majira ya kiangazi.

Taarifa zinadai kuwa Zidane anahofia kumtegemea sana Luka Modric katika nafasi ya kiungo na anataka kuimarisha safu hiyo kwa ajili ya msimu ujao.

Pogba ni aina ya mchezaji ambaye anaweza kucheza moja kwa moja katika kikosi cha kanza cha Madrid na Zidane ana matumaini ya kumnasa Mfaransa mwenzake huyo.

Tielemans kwa upande wake amekuwa katika kiwango bora toka alipoibuka katika kikosi cha kwanza cha Anderlecht na Madrid wanaona chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 18 ataweza kuisadia timu hiyo siku zijazo.