Oliseh ajiuzulu ukufunzi wa Nigeria

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Sunday Oliseh ajiuzulu ukufunzi wa Nigeria

Mkufunzi wa timu ya taifa la Nigeria Sunday Oliseh amejiuzulu wadhfa wake takriban miezi minane baada ya kupewa kazi hiyo.

Nahodha huyo wa zamani wa Super Eagles amelishtumu shirikisho la soka nchini Nigeria NFF kwa kushindwa kumlipa marupurupu yake.

Hakuna tamko lolote lililotolewa na shirikisho hilo ambalo viongozi wake wako mjini Zurich kwa uchaguzi wa rais wa FIFA.

Bwana Oliseh alitangaza kujiuzulu kwake katika mtandao wa Twitter.