Mwanariadha wa Ethiopia apigwa marufuku

Image caption Aregawi

Bingwa wa michezo ya ndani kwa ndani katika mbio za mita 1500 Abeba Aregawi amesimamishwa kwa mda kushiriki katika mchezo huo baada ya kupatikana na makosa ya kutumia dawa za kisisimua misuli.

Mwanariadha huyo wa Sweden aliyezaliwa nchini Ethiopia alipatikana na dawa hiyo baada ya kufanyiwa kipimo na shirikisho la riadha duniani IAAF.

Abeba, 25, alikimbilia Ethiopia katika michezo ya Olimpiki ya 2012 lakini akaanza kuiwakilisha Sweden baadaye mwaka huo baada ya kupewa uraia.

Marufuku yake inamaanisha kwamba nafasi yake katika kikosi cha Sweden katika mashindano ya Olimpiki ina utata.

Kamati ya Olimpiki ya Sweden tayari imeondoa ufadhili wake kwa mwanariadha huyo.