Tenisi:Konta, Watson watinga nane bora

Image caption Heather Watson atinga katika hatua ya nane bora ya michuano ya wazi ya Monterrey

Nyota wawili wa mchezo wa tenesi raia wa Uingereza Johanna Konta na Heather Watson, wametinga katika hatua ya nane bora ya michuano ya wazi ya Monterrey inayofanyika huko Mexico.

Konta anayeshika nafasi ya 27 kwa ubora wa viwango vya mchezo huo duniani alimfunga Yanina Wickmayer, wa Ubelgiji kwa seti 7-6 (8-6) 7-6 (7-4).

Kwa ushindi huo konta atachuana na na Mbeligiji mwingine Kirsten Flipkens au Alison van Uytvanck, ambae pia ni raia wa Ubeligiji.

Nae Heather Watson alipata ushindi wa seti 6-2 6-3, dhidi ya Polona Hercog wa Slovenia,hivyo mchezaji huyu atachuana na Caroline Wozniacki au Mirjana Lucic-Baroni katika raundi inayofuta.