Tottenham kuchuana na Arsenal

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Arsenal dhidi ya Tottenham

Kiungo wa kati wa Tottenham Mousa Dembele atashiriki katika mechi dhidi ya Arsenal baada ya kukosa mechi mbili akiuguza jeraha .

Mchezaji Dele Ali aidha huenda akaanza baada ya kutumika kama mchezaji wa ziada kutokana na jeraha dogo la kifundo cha mguu.

Wakati huohuo kipa wa Arsenal Petr Cech hatocheza kwa hadi wiki nne na jeraha la mguu alilopata baada ya kugongana na wachezaji wa Swansea wakati wa kupigwa kwa kona.

Mahala pake Cech patachukuliwa na David Ospina.Vilevile beki matata wa Arsenal Laurent Koscielny naye hatoshiriki kutokana na jeraha la paja.

Mechi nyengine zitakazochezwa katika ligi ya Uingereza siku ya jumamosi ni

Chelsea v Stoke

Everton v West Ham

Man City v Aston Villa

Newcastle v Bournemouth

Southampton v Sunderland

Swansea v Norwich

Watford v Leicester