Diamond League kufanyika barani Afrika

Haki miliki ya picha Getty

Mji wa Rabat utakuwa wa kwanza Afrika kuandaa mashindano ya riadha ya Diamond League, utakapokuwa mwenyeji wa mashindano hayo baadaye mwaka huu.

Jiji la New York hata hivyo limeondolewa kutoka kwenye mashindano hayo

Rabat, mji mkuu wa Morocco, utaandaa mashindano ya tatu ya msimu huu mnamo 22 Mei.

Rais wa Shirikisho la riadha duniani (IAAF) Lord Coe amesema kupitia taarifa: “Tuna furaha sana kupeleka mashindano haya makuu ya riadha hadi kwenye bara jingine.”

Waandalizi wa mashindano hayo jijini New York wamesema watajaribu kuandaa mashindano mengine badala ya Diamond League.

Haki miliki ya picha XINHUA
Image caption Wanariadha wakishindana mbio za Diamond League mjini Eugene

Marekani sasa imebaki na jiji moja pekee linaloandaa mashindano ya Diamond League, mji wa Eugene, Oregon.

Morocco imewahi kuandaa mashindano ya IAAF zamani, yakiwemo mashindano ya mabara ya 2014 mjini Marrakech.