Mshikemshike wa ligi ya Tanzania wikiendi

Image caption Timu ya Simba Sports nchini Tanzania

Ligi kuu ya Tanzania itaendelea tena mwisho wa wiki hii kwa nyasi za viwanja mbalimbali kuwaka moto.

Hapo kesho katika dimba la taifa Jijini Dar es Salaam kutachezwa mchezo wa wababe wawili wa soka Azam Fc watakaowakabili vinara wa ligi hiyo Yanga.

Huku African Sport wakiwa nyumbani katika uwanja wa mkwakwani kukipiga na Majimaji.

Toto Africans,watakua katika uwanja wa Kirumba, kupepetana na Ndanda FC. Kagera Sugar wao watakuwa na kibarua kizito dhidi ya Mgambo JKT.

Kikosi cha JKT Ruvu kitawaalika Mwadui Fc, toka Mkoani shinyanga wakati Wajelajela wa Tanzania Prisons watakua wenyeji wa Stand United, nao wakata miwa wa Mtibwa watapimana ubavu na Coastal Union.

Jumapili utapigwa mchezo mmoja ambapo Wekundu wa Msimbazi watakuwa na kibarua kizito cha kuwakabili Mbeya City mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.