MOJA KWA MOJA:Tottenham dhidi ya Arsenal

Tottenham inkabiliana na Arsenal katika debi ya london inayowavutia wengi huku timu zote mbili zikiwa miogoni mwa timu tatau bora katika jedwali la ligi ya Uingereza.

17.33pm:Wachezaji wa Arsenal wanasonga mbele licha ya kuwa chini kwa mchezaji mmoja aliyepewa kadi nyekundu.

17.30pm:lalala Beki Gabriel karibia ajifunge hapa akilinda lango lake.

17.29pm:Mpira wa adhabu kuelekea Tottenham na Alexi sancheza anapiga na kipa anaokoa lo

17.15pm:Totenham wanaanza kusonga mbele hapa lakini rsenal wanakataa

Image caption Mchezaji Alli Dele wa Tottenham na Bellerin wa Arsenal

Arsenal wacheza gusa ni guse na wanakaribia kupata bao hapa kupitia Weelbeck na sanchez lakini kipa anachukua.

17.07pm:Gooooooooooal Sanchez aifungia Arsenal bao la pili na kimarisha matumaini ya timu yake hapa

Image caption Harry Kane asherehekea bao lake

17.03pm:Goooooooooooal Tottenham yapata bao lao la pili baada ya dakika mbili na kuiweka kifua mbele Tottenham.Bao lililofungwa na Harry Kane

Tottenham 2-1 Arsenal

Image caption Lamela asherehekea bao lake

17.01pm:Gooooooooooooal Erick Lamelaaisawazishia Tottenham katika dakika 16 hapa

Tottenham 1-1 Arsenal

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Coquelin

16.57pm:Coquelin apewa kadi nyekundu hapa baada ya kumchezea visivyo mshambuliaji Harry Kane

16.55pm:Arsenal wanaonekana kumiliki mpira katika kipindi cha pili lakini mabeki wa Tottenham wamesimama wima

16.45pm:Kipindi cha pili cha mechi kati ya Tottenham dhidi ya arsenal chaanza.

16.32pm:Na kipindi cha kwanza cha mechi kati ya Tottenham na Arsenal kinakamilika

16.30pm:Arsenal sasa yaongeza ngu katika safu yake ya mashambulizi ikiwa ni dakika ya 45 hapa ya kipindi cha kwanza

Tottenham 0-1 Arsenal

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ramsey akifunga bao lake la kwanza

Goooooooal Arsenal wapata bao la kwanza hapa kupitia Ramsey baada ya guse ni guse

16.22pm:Kumbuka kwamba iwapo Arsenal itashindwa mechi ya leo basi itakuwa mechi ya nne kushindwa mfululizo wakati ambapo wanatarajiwa kukabiliana na Barcelona katika mechi ijayo ugani Cam Nou

16.19pm:Kona kuelekezwa lango la Tottenham lakini inapigwa na kurudi lango la Arsenal.Anachukua Bellerin na kumpatia kipa Ospina ambaye anaupigwa mbele

Arsenal inaanza mashambulizi hapa kupitia Wellbeck lakini Kipa Hugo Lloris anaokoa.

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Arsenal dhidi ya Tottenham

16.15pm:Dakika ya 30 inaingia Tottenham 0-0Arsenal

16.14pm:Lamela anapewa kadi ya njano baada ya kucheza visivyo

Mpira wa adhabu unapigwa kuelekea lango la Arsenal baada ya Bellerin kumuangusha mchezaji wa Tottenham lakini Kipa Ospina autia mkobani mpira ule.

16.06pm:Tottenham yafanya mashambulizi hapa lakini David Ospina anaokoa kwa upande wa Arsenal.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Harry Kane akijaribu kuipenya ngome ya Arsenal

16.04pm:Vijana wa Wenger wanaonekana kujaribu kwenda mbele lakini hawana kasi ya mpira wanapowasili katika lango la Tottenham.

16.02pm:Mpira mwengine wa adhabu unapigwa kuelekezwa lango la Arsenal lakini unakwenda moja kwa moja kwa golkipa Ospina

16.00pm:Namuona Dembele hapa akimiliki safu ya kati ya Arsenal

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Tottenham dhidi ya Arsenal

15.59pm:Mpira wa adhabu kuelekea lango la Arsenal.Arsenal wanazuia pale na mpira unatoka nje

15.47pm:Tottenham wanaoneka wakianza mechi kwa kasi kupitia Ali Delle na Harry Kane.

Image caption Tottenham

kikosi cha Tottenham

15.45pm:Mechi kati ya Arsenal dhidi ya Tottenham imeanza

Image caption Arsenal

Kikosi cha Arsenal