Pellegrini:Tunahitaji kushinda mechi 9

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Pellegrini

Manchester City italazimika kushinda mechi tisa kati 11 zilizosalia ili kuweza kushinda taji la ligi ya Uingereza,Mkufunzi Manuel Pellegrini amesema.

Manchester City ambayo iko katika nafasi ya nne iko pointi kumi nyuma ya viongozi wa ligi Leicester baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo.

Pellegrini anahisi kwamba pointi 75 zitaisaidia timu yake kushinda taji la ligi ,jumla ambayo timu yake iko nyuma na pointi 28 kuafikia.

''Tumekuwa na wakati mbaya lakini tuna pointi 33 za kujaribu kuafikia lengo hilo,''alisema Pellegrini.

''Nilisema miezi kadhaa iliopita kabla ya kumaliza awamu ya kwanza ya mechi kwamba huenda mshindi wa ligi akapata chini ya pointi 80.Huwezi kubaini kwa sasa lakini nadhani mshindi atakuwa na alama 75 ama zaidi''.