Samata kuiongoza Taifa Stars AFCON

Image caption Nahodha ni Mbwana Samatta (KRC Genk),

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ametangaza kikosi cha wa wachezaji 25 kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Chad.

Mechi hiyo imeratibiwa kusakatwa tarehe 23 Machi mjini Djamena.

Image caption Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa

Akiongea na waandishi wa habari wakati akitangaza kikosi hicho, Mkwasa, amewaomba wachezaji aliowaita katika kikosi hicho, kujiweka katika hali nzuri ya mazoezi katika vilabu vyao, kwani hakutakua na muda wa kufanya mazoezi kwa ajili ya mchezo huo wa ugenini.

Wachezaji walioitwa Taifa Stars ni magolikipa Aishi Manula (Azam FC), Ally Mustapha (Young Africans) na Shaban Kado (Mwadui FC), walinzi ni Juma Abdul, Haji Mwinyi, Kelvin Yondani (Young Africans), Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, David Mwantika (Azam FC) na Mohamed Hussein (Simba SC).

Image caption Taifa Stars mpya ya AFCON yatajwa

Viungo Himdi Mao (Azam FC), Ismail Juma (JKU), Jonas Mkude, Said Ndemla, Mwinyi Kazimoto (Simba SC), Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar), Farid Mussa (Azam FC), Deus Kaseke (Young Africans).

Washambuliaji ni Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe), John Bocco (Azam FC), Elias Maguri (Stand United), Jeremia Mgunda (Tanzania Prisons) na Ibrahim Hajibu (Simba SC).