Liverpool kuchuana na Man United Europa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Louis Van Gaal

Mkufunzi wa timu ya Liverpool Jurgen Klopp ameitaja mechi ya Alhamisi ya kombe la Europa kati ya Liverpool na Manchster United kuwa mechi kubwa sana.

Liverpool wanaikaribisha Anfield timu ya Manchester United ikiwa ni mkutano wao wa kwanza Ulaya.

Hatahivyo Klopp anasema :''kila siku kombe la Europa linafurahisha.Ni Mechi kubwa sana.Ijapokuwa sio kubwa zaidi katika kazi yangu kama mkufunzi wa Liverpool lakini ni muhimu sana''.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Liverpool

Manchester United imeshinda makombe 3 ya bara Europa hivi karibuni ikiwa 2008,huku Liverpool ikilibeba kombe hilo mara tano.

Mkufunzi wa Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa wale wanaomkosoa kwa kushushwa katika kombe la Europa hawaelewi huku Klopp akisema kuwa anaamini mechi hiyo itasisimua mashabiki katika uwanja wa Anfield.