Spurs,United chali Europa ligi

Image caption Tottenham vs Hotspur

Tottenham Hotspurs wakicheza ugenini katika dimba Signal Iduna Park huko nchi Ujeruman wamekubali kichapo cha mabao 3-0 .

Pierre-Emerick Aubameyang ndie aliyeanza kuifunga Spurs kwa bao la dakika 30 kisha mchezaji bora wa mchezo huo Marco Reus akafunga mabao mengine mawili katika dakika ya 61 na 70.

Nao Mashetani wekundu wa Man United wakachapwa kwa mabao 2-0 na Liverpool katika mchezo uliopigwa katika dimba la Anfield, Dany Sturridge, alifunga goli la kwanza kwa mkwaju wa penati kisha Roberto Firmino akafunga bao la pili.

Matokeo ya michezo mingine

Valencia 0-1 Athletic Bilbao

Basel 0-0 Sevilla

Fenerbah├že 1-0 Sporting Braga

Shakhtar Donetsk 3-1 Anderlecht

Sparta Prague 1-1Lazio

Villarreal 2-0 Bayer 04 Leverkusen