Aguero kuihama Man City 2019

Image caption Sergio Aguero

Mshambuliaji wa kilabu ya Manchester City Sergio Aguero amesema kuwa atakihama kilabu hicho wakati kandarasi yake itakapokamilika.

Rais huyo wa Argentina ana kandarasi ya miaka mitano na uwanja wa Etihad atakamilisha kandarasi yake katika msimu wa 2018-19.

Ameifungia City mabao 128 tangu aliposajiliwa na kilabu hiyo kutoka Atletico Madrid kwa kitita cha pauni milioni 38 mwaka 2011,na kushinda ubingwa wa ligi ya Uingereza mara mbili.

Aguero mwenye umri wa miaka 27 alikiambia kituo kimoja cha redio nchini Argentina kwamba ni wazi atarudi katika kilabu yake ya kwanza ya Independente na kustaafu.

''Hapa City wanajua ni nini ninacho taka kufanya,wanajua nataka kurudi Argentina'',aliongezea.