Liverpool yailaza Manchester United Europa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kipa De Gea wa Manchester United akiokoa mashambulizi

Liverpool ilichukua udhibiti wa kombe la bara Europa baada ya kuifunga timu ya Manchester United iliokuwa ''haijiwezi'' katika uwanja wa Anfield.

Kilabu ya kocha Jurgen Klopp ilitawala awamu ya kwanza ya mchuano huo katika mazingira yaliojaa mashabiki wengi.

Danniel Sturidge aliifungia Liverpool bao la kwanza kunako dakika ya 20 baada ya mchezaji wa Manchester United Memphis Depay kumuangusha Nathaniel Clyne kabla ya Roberto Firmino kuongeza bao la pili akiwa karibu na goli ikiwa imesalia dakika 17 pekee.

United hawakupata hata nafasi moja na ni mchezo mzuri wa kipa De gea uliozuia mashambulizi ya Liverpool.