Olimpiki:Mabondia wa Uganda washinda

Image caption Bondia Japhet Kaseba

Uganda wameshinda mapigano ya ufunguzi jana katika mashindano ya Africa ya kufuzu kwa michezo ya Olimpiki.

Sulaima Segawa uzani wa light alimtandika vilivyo Stephen Kabelo wa Botswana kwa pointing 3-0,huku Kennedy Katende akimpondaponda Yoada Aboubacar wa Ivory Coast kwa pointi 3-0.

Bondia mwingine wa Uganda Willy Kyakonye uzani wa heavy alishindwa na David Akankolim kwa TKO raundi ya kwanza.

Leo hii mabondia wa eneo hili watakaozipiga ni Sulaiman Segawa,Michael Sekabembe uzani wa super-heavy wote wa Uganda,Nick Okoth uzani wa light na Fred Otieno uzani wa super-heavy wote wa Kenya na Biru Mesfin wa Ethiopia uzani wa light.

Tanzania ilijiondoa mashindanoni kwa sababu ya uhaba wa fedha.