Van Gaal: Mbinu yetu inafua dafu

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Louis Van Gaal

Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis Van Gaal amesisitiza kuwa mbinu yake ya uchezaji katika kilabu yake imeanza kufua dafu,huku kilabu hiyo ikiwa inaendelea kushindana katika makombe matatu.

United ambayo iko katika nafasi ya sita iko pointi tatu nyuma ya nafasi ya kushiriki katika kombe la vilabu bingwa na inaialika kilabu ya West Ham kwa mechi ya kombe la FA siku ya jumapili.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Louis Van Gaal

Liverpool baadaye itaelekea katika uwanja wa Old Trafford siku ya Alhamisi ,huku United ikijaribu kubadilisha matokeo ya 2-0 ili kuweza kufuzu kwa robo fainali ya michuano hiyo ya Europa.

''Nadhani mbinu hiyo inafanya kazi ,alisema Van Gaal,akikana madai kwamba kilabu hiyo imefali katika uongozi wake.Hatupati matokeo mazuri sana.Sio mazuri sana ukifikiria kwamba ni lazima uwe bingwa wa ligi,ushinde kombe la bara Europa ama upate ushindi wa kombe la FA.Kuna wenzetu wengi ambao hawapiganii makombe matatu''.