Manchester City kukabili Kiev UEFA

Haki miliki ya picha Getty

Michuano ya klabu bingwa barani ulaya inatarajia kuendelea tena leo Jumanne kwa michezo Miwili.

Atletico Madrid watakuwa wenyeji wa PSV Eindovein ya Uholanzi, na Manchester City ya Uingereza watakuwa nyumbani Etihad wakiwaalika Dianamo Kiev ya Ukraine.

Michuano hiyo itaendelea tena kesho Jumatano kwa mechi mbili, Barcelona watakuwa wenyeji wa Arsenal, na Bayern Munich wataikabili Juventus.

Fainali za michuano hiyo zitahitimishwa tarehe 28 mwezi Mei 2016 uwanja wa San Siro mjini Milan nchini Italia.