Gallacher kufanyiwa upasuaji mkono.

Haki miliki ya picha Getty

Mchezaji Golf Stephen Gallacher atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja kutokana na maumivu mkono.

Mshindi huyo wa Michuano ya Ryder Cup 2014 amesema amekuwa akisumbuliwa na tatizo hilo muda mrefu na kumlazimu kuwa nje ya michuano PGA.

Gallacher mwenye umri wa miaka 41, anatarajia kurejea katika katika michuano ya wazi ya Hispania mjini Valderrama mwezi Aprili.