Twiga stars kuwafuata Wazimbabwe.

Timu ya Taifa ya soka ya wanawake ya Tanzania inatarajiwa kusafiri Ijumaa kuelekea Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa marudiano.

''Twiga Stars'' inawania kufuzu fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake zitakazofanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini Cameroon.

Kikosi cha Twiga Stars kinaendelea na mazoezi katika uwanja wa Karume chini ya kocha mkuu, Nasra Juma kujiandaa na mchezo huo muhimu ili kuweza kusonga mbele katika hatua inayofuata.

Kuhusu maendeleo ya kambi, kocha Nasra Juma amesema vijana wake wanaendela vizuri, wamekua wakiendelea na mazoezi tangu baada ya mchezo wa awali na ana imani watafanya vizuri katika mchezo wa marudiano.

Twiga Stars inahitaji ushindi katika mchezo huo utakaochezwa Jumapili, Machi 20 katika uwanja wa Rufalo uliopo jijini Harare ili kuweza kufuzu kwa hatua ya pili ya michuano hiyo.

Katika mchezo wa awali uliopigwa jijini Dar es salaam uwanja wa Azam, Twiga stars walikubali kipigo cha bao 2-1