Robo fainali Uefa Champion kujulikana.

Image caption Uefa champions

Timu nane toka nchi tano leo Ijumaa zitatumbukizwa kwenye Chungu kimoja kwenye droo ya kupanga mechi za robo fainali ya Uefa championi Ligi shughuli itakayofanyika huko Nyon, Uswisi. Droo hii iko wazi ikimaanisha timu za nchi moja zinaweza kukutanishwa na hivyo upo uwezekano wa, mathalani, Real Madrid na Barcelona kukutana. Klabu zilizofuzu kuingia robo fainali ni Atl├ętico Madrid,Bayern Munchen, Barcelona,Benfica,Manchester City,Paris Saint-Germain,Real Madrid na Wolfsburg. Mechi za Robo Fainali zitachezwa Tarehe Aprili 5 na 6 na Marudiano ni Aprili 12 na 13.