MOJA KWA MOJA:Everton dhidi ya Arsenal

Arsenal inakabiliana na Everton katika mechi ya ligi kuu ya Uingereza.

17.39pm:Na mechi inakamilika huku Arsenal wakiibuka washindi baada ya kuishinda Everton 2-0 .

Image caption Mchezaji wa Arsenal Hector Bellerin

17.37pm:Arsenal wanacheza mchezo mzuri lakini swali ni je,wataweza kucheza hivyo kwa kipindi cha msimu kilichosalia?

17.36pm:Arsenal wanavia lango la Everton lakini Giroud anapiga nje

17.35pm:Kona inapigwa kuelekezwa lango la Arsenal lakini kipa Davdi Ospina anachukua mpira ule maridadi.

Image caption Ozil

17.32pm:Everton inatafuta bao kwa udi na uvumba lakini bahati haijasimama.Wanapata kona pale everton.

17.30pm:Iwobi atoka na badala yake Chamberlain anaingia

17.24pm:Goooooooal Giroud anafunga lakini refa anakataa na kusema alicheza visivyo.Dakika za lala salama Everton 0-2 Arsenal

Image caption Wellbeck

17.18pm:Wellbeck atoka na Giroud aingia

17.17pm:Arsenal wanaonekana wakitaka kufanya mabadiliko baada ya Ozil kukanyagwa pale huku kipa david Ospina pia akionekana kwamba bado hali yake sio nzuri.Everton wafanya mabadiliko Barclays aotoka

17.16pm:Vijana wa Everton wazidi kulishambulia lango la Arsenal

Image caption david Ospina baada ya kujeruhiwa na Lukaku

17.13pm:Everton sasa imevamia lango la Arsenal baada ya kipa wa Arsenal David Ospina kuumia.Inaonekana kwamba huenda asiimalize mechi hii.

Image caption Lukaku na El-Neny

17.05pm:Everton wameanza kuamka lakini bnado Arsenal inaendelea kudhibiti mechi.

16.45pm:Arsenal bado wanaendelea kutawala mpira dhidi ya Everton licha ya washambuliaji wake Romeo Lukaku na barclays kujaribu kupenya lango la Arsenal

Kipindi cha pili cha mechi

16.28pm:Gooooooooooooal Alexi Iwobi aifungia Arsenal bao la pili hapa dhidi ya Everton Everton 0-2 Arsenal 43''

Image caption Bellerin

16.26pm:Wachezaji barclays na LUkaku wamepotezwa na huonekana mara moja moja wakati Everton inapovamia lango la Arsenal.

16.25pm:Everton na mpira .Wanajaribi kugusa gusa katika lango la Arsenal.Kona kuelekezwa lango la Arsenal.

16.22pm:Sanchez analalamika hapa baada ya kudai kuangushwa katika eneo la hatari.

Image caption Arsenal dhidi ya Everton

16.16pm:Lukaku anajaribu kuivunja ile ngome ya Arsenal lakini mabki wanakataa

16.15pm:Everton inapiga kona lakini Arsenal wanaupiga mbele mpiravkuelekea lango la Everton.

16.10pm:Everton washambulia hapa lakini beki wa Arsenal autoa mpira.Konakuelekezwa Arsenal

Image caption sanchez

16.09pm:Everton sasa kupitia Baines apiga krosi safi hapa na Ospina audoka na kumtoka minoni lakini aurukia na kuutuliza mpira kabla ya kutoka.

16.08pm:Arsenal wapata kona pale ,lakini mpira unakuwa mwingi na kutoka baada ya Ozil kumpatia pasi Wellbeck

15.59pm:Arsenal wanaendelea kutawala mechi huku wachezaji wa kiungo cha kati wakitawala safu hiyo na kuwawacha wachezaji wa Everton bila jibu.

Image caption Wellbeck akifunga

15.56pm:Goooooooal Arsenal yajipatia bao la kwanza baada ya gusa ni guse kati ya Welbeck,Ozil na Sanchez.

15.45pm:Mechi inaanza kwa kasi huku timu zote mbili zikishambulia lango la upinzani.