Azarenka amshinda Serena

Image caption Victoria Azarenka alipata ushindi wa seti 6-4 6-4 dhidi ya Serena Williams

Nyota wa mchezo wa tenesi Victoria Azarenka amemshinda mpinzani wake Serena Williams na kutwaa ubingwa wa michuano ya wazi ya BNP Paribas.

Azarenka alipata ushindi wa seti 6-4 6-4 katika mchezo mgumu dhidi ya nyota namba moja kwa ubora wa mchezo .

Baada ya kupata ushindi huu nyota huyu wa tenesi atarejea katika nafasi ya kumi bora katika viwango vya ubora kuanzia jumatatu hii.

Na huu umekua ni ushindi wanne kwa Azarenka mwenye 26 katika michezo 21 waliyowahi kukutana na Serena.