Mashabiki 2 wa Raja Casablanca wauawa

Image caption Mashabiki 2 wa Raja Casablanca wauawa

Mashabiki wawili wa kandanda walifariki dunia siku ya jumamosi baada ya mechi kali kati ya Raja de Casablanca ya Morocco na klabu ya Chabab Rif Al Hoceima.

Msemaji wa shirikisho la soka la nchi hiyo (FMRFF) ameiambia BBC.

Mashabiki walifokeana hata kabla ya mechi hiyo kuanza katika uwanja wa Mohammed wa Tano .

Hadi kufikia sasa haijajulikana kilichoibua uhasama huo miongoni mwa mashabiki wa Raja ambao walinaswa na kamera fiche wakivunja na kuharibu mali ya uwanja huo licha ya timu yao kuitandika Chabab Rif Al Hoceima mabao 2-1.

Utawala unasema kuwa watu zaidi ya 31 walikamatwa kufuatia machafuko hayo.

Klabu ya Raja nayo haikusazwa.

Imepigwa faini ya diham laki moja sawa na pauni elfu saba.

Vile vile Raja sasa italazimika kucheza mechi zake 5 zijazo pasi na mashabiki.