Usmanov: Arsenal ''inamuhitaji'' Arsene Wenger

Haki miliki ya picha RIA Novosti
Image caption Bilionea Alisher Usmanov

Arsenal ''inamuhitaji'' Arsene Wenger hivyobasi mkufunzi huyo wa The Gunners ana uwezo wa kumchagua mrithi wake wakati atakapoondoka,kulingana na mwanahisa mkuu wa klabu hiyo Alisher Usmanov.

Wenger pia lazima ashiriki katika ''kumteua mrithi wake''.

''Kilabu hiyo lazima iendelee chini ya ukufunzi wa ''nembo yake na mali yake'' ambaye ni mkufunzi ''Arsene Wenger', alisema mfanyibiashara huyo wa Urusi.

Lakini licha ya kumuunga mkono Usmanov aliongezea kwamba Arsenal imekabiliwa na tatizo la kushindwa kushinda mataji kwa miaka mingi na ''haiwezi kushinda taji la ligi kuu ya Uingereza msimu huu''.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Arsene Wenger

Arsenal tayari imeondolewa katika mashindano ya vilabu bingwa Ulaya katika harakati za kutaka kufuzu katika robo fainali na kupoteza dhidi ya Watford katika robofainali ya kombe la FA.

Kwa sasa wako katika nafasi ya tatu katika ligi ya Uingereza wakiwa na pointi 11 nyuma ya viongozi Leceister na hawajashinda taji la ligi tangu mwaka 2004.