Salah ainusuru Misri dhidi ya Nigeria

Image caption Mohammed Salah

Mohammed Salah alifunga katika dakika za majeruhi na kuinusuru Misri kupata pointi moja ugenini dhidi ya Nigeria katika mechi ya kufuzu kwa kombe la Afrika mwaka 2017.

Matokeo hayo sasa yanaiweka Misri katika kilele cha kundi G ikiwa na pointi mbili juu ya Nigeria.

The Super Eagles walichukua uongozi kupitia mshambuliaji wa timu ya Warri Wolves Etebo Oghenekaro lakini kiungo wa kati wa Roma Salah akasawazisha katika dakika ya 91.

Timu mbili za juu katika kila kundi zina fursa ya kufuzu katika raundi ya pili katika harakati za kuelekea Gabon 2017.