Suarez aisawazishia Uruguay dhidi ya Brazil

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Luis Suarez

Luis Suarez alifunga bao la pili na kuisawazishia Uruguay katika kipindi cha pili katika droo ya 2-2 dhidi ya Brazil katika mechi yake ya kwanza ya kimataifa tangu apigwe marufuku kwa kumng'ata mchezaji mwenzake katika kombe la dunia la mwaka 2014.

Mshambuliaji huyo wa Barcelona alikuwa hajaichezea Uruguay katika mechi ya kimataifa kwa takriban siku 640 kabla ya mechi ya kufuzu ya kombe la dunia siku ya Ijumaa.

Douglas Costa aliifungia Brazil baada ya sekunde 39 kabla ya Renato Augusto kuongeza uongozi huo katika dakika ya 26.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Suarez baada ya kumng'ata Chiellini

Hatahivyo Edison Cavani aliifungia Uruguay bao la kwanza kabla ya Suarez kufunga la pili baada ya kipindi cha kwanza.

Suarez ambaye alikiongoza kikosi hicho katika uwanja wa Itapeva Arena Pernambuco,alimng'ata sikio mlinzi wa timu ya Italy Giorgio Chiellini wakati wa mechi ya mwisho ya kimakundi katika kombe la dunia mnamo mwezi Juni mwaka 2014.