Bondia Adrien Broner apokonywa taji

Image caption Adrien Broner

Bondia Adrien Broner wa Marekani amepokonywa taji lake la WBA uzani wa Light Welter weight baada ya kushindwa kujipima kwa maandalizi ya pigano lake dhidi ya Muingereza Ashley Theophane siku ya Ijumaa.

Broner mwenye umri wa miaka 26 alikuwa na uzito wa pauni 140.4 na alikuwa na saa mbili kupunguza uzito huo lakini akashindwa kurudi katika upimaji huo.

Alitarajiwa kutetea taji lake dhidi ya Theophane mjini Washington.

Hatahivyo pigano hilo litaendelea na ni bondia huyo wa Uingereza atakayeruhusiwa kuchukua ukanda huo iwapo atashinda.

Ni mara ya pili kwa Broner kupokonywa taji lake.

Alipoteza taji jingine la WBO uzani wa Super Featherweight mwaka 2010 kwa kushindwa kuafikia mahitaji ya uzani wa pigano dhidi ya Vicente Escobedo.