Wenger: Matamshi ya Ozil hayakubaliki

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Arsene Wenger

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amesema kuwa matamshi ya Mesut Ozil kuhusu msimu mbaya wa Arsenal hayakubaliki.

Wenger atazungumza na mchezaji huyo wa Ujerumani anayesema kuwa Arsenal imepoteza fursa ya kushinda taji la Uingereza.

''Nakubaliana kwamba matamshi hayo hayaungwi mkono'' ,alisema Wenger.

''Hata iwapo tuna fursa moja pekee dhidi ya 100 lazima tuamini''.

Ushindi wa mechi tatu kati ya 10 katika ligi ya Uingereza umeiwacha Arsenal ikiwa pointi 11 nyuma ya viongozi Leicester wakiwa na mechi moja ambayo hawajacheza.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mesut Ozil

Arsenal inakabiliana na Watford siku ya Jumamosi ikiwa ni marudio ya mechi ya kombe la FA ambapo Watford ilishinda na kuibandua Arsenal.

''Kitu kibaya katika maisha ni kutojiamini.Lazima uhakikishe kuwa unajitolea vilivyo na mwishowe ukubali iwapo mpinzani wako ni mzuri kukuliko''.