Yanga yashinda, Azam yavutwa shati

Image caption Kikosi cha watoto wa Jangwani Yanga.

Ligi kuu ya Tanzania bara iliendelea tena mwisho wa wiki kwa michezo mitano kupigwa.

Katika dimba la Taifa Jijini Dar Es Salaam klabu ya soka ya Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Kagera Sugar.

Mabao ya wanajangwani hao yalifungwa na Donald Ngoma, Amisi Tabwe na mlinzi wa kushoto haji Mwinyi akifunga bao la mwisho,huku bao pekee la Kagera Sugar likifungwa na Mbaraka Yussuf.

Nao Azam Fc wakicheza ugenini kwenye dimba la Kirumba huko Mkoani Mwanza walikwenda sare ya bao 1-1 na Toto Africans.

Matokeo ya michezo mingine ni

Stand United 2 – 0 Mgambo JKT

Ndanda FC 0 – 0 Tanzania Prisons

JKT Ruvu 1 – 0 African Sports