Rosberg ashinda taji Bahrain

Haki miliki ya picha AP
Image caption Nico Rosberg

Dereva wa magari yaendayo kasi ya Formula Nico Rosberg wa timu ya Mercedes ametwaa ubingwa wa michuano ya Bahrain Grand Prix.

Rosberg alipata ushindi huku akimzidi dereva mwenza wa timu yake Mwingereza Lewis Hamilton ambae gari lake liligonga na katika raundi ya kwanza.

Dereva wa timu ya Ferrari Kimi Raikkonen alisika nafasi ya pili katika michuano hiyo.Huku Lewis Hamilton akiambulia nafasi ya tatu.

Ushindi wa dereva huyu ni watano mfululizo na kumpa nafasi ya kuongoza kwa alama 17 mbele ya Lewis Hamilton.