Serengeti boys kuwakabili Mafarao Kesho

Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri 17 kesho watashuka dimbani kucheza mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya timu ya Misri Mafarao.

Mchezo huo utachezwa kwenye uwanja wa Azam Complex, ni mchezo wa marudiano ambapo mchezo wa kwanza ulichezwa jumamosi iliyopita katika uwanja wa Taifa Jijini Dar Es Salaa.

Mchezo utachezwa saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki na Kati, Katika mchezo wa kwanza Serengeti boy walishinda kwa ushindi wa mabao 2-1

Mchezo huo wa kirafiki ni sehemu ya maaandalizi kwa timu zote Tanzania (U17) na Misri (U17) zinazojiandaa na michezo ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Vijana mwaka 2017 zitakazofanyika nchini Madagascar.