Watson apoteza mchezo

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Heather Watson

Nyota wa Tenesi raia wa Uingereza, Heather Watson ameanza vibaya michuano ya wazi ya Katowice inayofanyika huko nchi Poland.

Watson amepoteza mchezo wa raundi ya kwanza ya michuano hiyo kwa kupoteza kwa 6-2 3-6 6-4 dhidi ya Kristyna Pliskova wa Jamuhuri ya Czech.

Nyota huyu tenesi wa Uingereza mwenye umri wa miaka 23 anashika nafasi ya pili kwa ubora nchi kwao huku akishika nafasi ya 55 kwa ubora wa dunia.

Pliskova anashika nafasi ya 88 kwa viwango vya ubora vya mchezo wa tenesi kwa upande wa wanawake.