Die nje mpaka mwisho wa msimu

Haki miliki ya picha AFP

Kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast anayechezea klabu ya Stuttgart atakua nje ya dimba mpaka mwisho wa msimu.

Die mwenye umri wa miaka 32 anasumbuliwa na maumivu ya mguu aliomua wakati wa mchezo dhidi ya Darmstadt mchezo uliochezwa jumamosi iliyopita.

Mkurugenzi wa michezo wa Stuttgart amesema "Hii ni bahati mbaya sana , Serey Die ni mpiganaji na tunasikitika tutamkosa "

Pia kiungo huyu atakosa mchezo wa kirafiki wa timu yake ya taifa dhidi ya Gabon utaopigwa mwezi June.