Higuain afungiwa mechi nne

Haki miliki ya picha Reuters

Mshambuliaji wa klabu ya Napoli Muargentina Gonzalo Higuain amefungiwa mechi 4 kwa kosa la kumsukuma mwamuzi katika mchezo dhidi ya Udinese uliofanyika jumamosi iliyopita.

Mbali ya Kifungo cha michezo hiyo 4 mshambuliaji huyu, ametozwa faini ya kiasi Euro 20,000.

Katika mchezo huo Higuian alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kupata Kadi za Njano ya Pili kwa kumcheza faulo Felipe wa Udinese.

Kukosekana kwa mshambuliaji huyo kutoka Argentina ni pigo kwa Napoli ambao wanagombea Ubingwa wa Italy wakiwa na alama 6.

Adhabu hii itamfanya Higuian kukosa michezo dhidi ya Verona, Inter Milan, Bologna na ule wa As Roma.