Serengeti boys yawachapa Mafarao

Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 17 imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya mafarao wadogo wa Misri.

Mabao ya Serengeti Boys yalifungwa na Ibrahim Abdallah aliefunga mabao mawili na Boko Selemani akifunga moja Huku mabao ya mafarao yakifungwa na Mostafa Elyas na Diaa Wahid.

Hii ni mara ya pili kwa Timu hizi kupambana na katika Mchezo wa awali uliochezwa Jumamosi katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam, Serengeti Boys waliibuka na ushindi wa mabao 2 – 1.

Michezo hii ya kirafiki ni sehemu ya maaandalizi kwa Timu zote mbili zinazojiandaa na kufuzu kucheza Fainali za Mataifa Afrika kwa Vijana mwaka 2017 zitakazofanyika nchini Madagascar.

Kwenye Mashindano hayo katika Mechi za Mchujo Serengeti Boys itaivaa Shelisheli hapo Juni 25, 2016 katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam na marudiano kuchezwa baada ya Wiki moja nchini Shelisheli.