MOJA KWA MOJA: West Ham dhidi ya Arsenal

Kilabu ya West ham inakabiliana na Arsenal wakati ambapo ligi ianelekea kukamilika huku kukiwa na mechi saba zilizosalia.Arsenal inawania kushinda taji la ligi huku West Ham nayo ikiwania uwakilishi katika kombe la vilabu bingwa Ulaya.Sunderland 1-0 Newcastle16.39pm:Na Mechi inakamilika hapa ikiwa West Ham 3-3 Arsenal 16.36pm:Kwa kweli hakuna timu inayocheza na wachezaji wa safu ya kati maana kila mara ni mashambulizi

16.26pm:Sanchez achenga hadi ndani ya lango la West ham laki afanya madoido na kukjosa bao la wazi

16.21pm:West Ham wanafanya mashambulizi hapa kupitia Payet ,Caroll na Crossroad lakini bahati haijasimama hapa.

Image caption Koscielny

16.14pm:Gooooooooooooal Koscielny aipatia Arsenal bao la tatu hapa dhidi ya West Ham

West Ham 3-3 Arsenal

16.01pm:West Ham sasa inatawala mchezo hapa ikiendelea kuwa kifua mbele

Image caption Andy Caroll

15.58pm:Goooooooooal West Ham inapata bao lake la tatu hapa kupitia Andy Caroll

Kipindi cha pili na West Ham inaanza kwa kasi hapa ikifanya mashambulizi chungu nzima.

Image caption Andy Caroll aifungia West Ham

15.34pm:Kipindi cha kwanza cha mechi kinakamilika

West Ham 2-2 Arsenal

15.33pm:Goooooooooooal Andy Caroll aipatia West Ham bao la pili

Image caption Andy Caroll

15.31pm:Gooooooooal Andy Carol aipatia West ham bao la kwanza hapa katika dakika ya mwisgho ya kipndi cha kwanza

15.25pm:West Ham wakosa bao hapa kupitia mchezaji wao Andy Caroll baada ya mlinda lango wa Arsenal David Ospina kuutema mpira na kuudaka

15.21pm:Gooooooooal Arsenal wajipatia bao la pili hapa kupitia Alexi Sanchez

West ham 0-2 Arsenal

15.16pm:Dakika ya 31 West 0-1 Arsenal

Arsenal inashambulia kwa kasi sana hapa .Mchezaji Payet wa West Ham anonekana kuwasumbua walinzi wa Arsenal

15.13pm:West yatafuta bao hapa kwa udi na uvumba.Na payet apata mkwaju wa dhabu,anapiga lakini walinzi wa Arsenal wakataa.

Image caption Ozil

15.04pm:Goooooooooooal Ozil aipatia Arsenal bao la kwanza hapa baada ya mashambulizi katika lango la West Ham

15.01pm:la la la Welbeck apata pasi nzuri kutoka kwa Iwobi lakini walinzi wa West hama wasimama wima na kuutoa mpira

15.00pm:Gooooooal West ham wajiweka kifua mbele lakini refa asema ameotea.lingekuwa bao zuri sana

Kumbuka kwamba West haijawahi kufungwa nyumbani katika shindano lolote.

Image caption Koscielny vs Andy Caroll

14.57pm:West Ham sasa inadhibiti mpira na kutafuta njia ya kuikabili Arsenal.

14.55pm:Timu zote zinaonyesha umahiri wao hapa,ijapokuwa Arsenal wanaonekana wakicheza na kushambulia kwa kasi.

14.49pm:Andy Caroll apokea kadi ya mapema ya manjano baada ya kumchezea visivyo Kolscieny

14.46pm:West Ham waanza na moto na wanakosa bao la mapema hapa

14.45pm: Mechi kati ya West Ham dhidi ya Arsenal Inaanza

Image caption West Ham
Image caption Arsenal
14.42pm:West Ham dhidi ya Arsenal