Bondia Anthony atamba kupigana na Fury

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Anthony Joshua alitwaa mkanda wa IBF wa dunia uzani wa Heavyweight

Bondia Anthony Joshua amesema sasa macho na akili zake anazielekeza kwa bondia Tyson Fury hii ni baada ya kushinda mkanda wa IBF wa dunia uzani wa Heavyweight siku ya Jumamosi na katika raundi ya pili ya mtoano ya dhidi ya mpinzani Charles Martin.

Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 26 ambaye ni bingwa wa Olimpiki amesema sasa anahitaji kupambana na bondia Fury na kuendelea kutetea mataji.