UEFA: Man City kuikabili PSG

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mechi za marudiano UEFA kupigwa jumanne na Jumatano

Mechi za Marudiano za Robo Fainali ya michuano ya Uefa zinaendelea tena Jumanne na jumatano kwa michezo minne, ambapo jumanne kutachezwa mechi mbili .

Manchester City watakuwa wenyeji wa Paris St-Germain katika dimba lao la Etihad na huko Santiago Bernabeu Real Madrid wako kwenye kibarua kigumu cha kugeuza kichapo cha 2-0 toka VfL Wolf-sburg walichokipata wiki iliyopita

Siku ya Jumatano Benfica watawakaribisha Bayern Munich ,na Atletico Madrid watakuwa wenyeji wa Barcelona.