Didier Drogba akaribisha uchunguzi

Image caption Didier Drogba

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba, amekaribisha uchunguzi ufanywe juu ya taasisi yake dhidi ya kile kilichoitwa "wasiwasi mkubwa juu ya udhibiti".

Gazeti la Uingeza limedai kuwa kiasi cha paundi 14,115 nje ya paundi 1.7 ilizochangiwa taasisi ya Didier Drogba kama hisani ndizo zilizosaidia Barani Afrika.

Tume ya taasisi hiyo imefungua kesi kufanya mapitio ya wasiwasi huo dhidi ya utawala la taasisi hiyo,lakini Drogda mwenye umri wa miaka 38 amesema hana mashaka, kwani kila kitu kiko sawa na pesa hizo zinaweza kutumika pale itakabidi kutumika .

Katika makala iliyoandikwa kwenye gazeti hilo linaeleza kuwa paundi 439,321 zilitumika katika sherehe za anasa za kifahari kutafuta fedha ambazo zilihudhuriwa na watu maarufu,na zaidi ya paundi milioni moja zimezuiliwa katika akaunti ya benki.