Michael Jamieson kuacha kuogelea

Image caption Michael Jameson

Muogeleaji Michael Jamieson huenda akastafuu mchezo huu baada ya kushindwa kufuzu kupata tiketi ya kushiriki michuano ya Olimpic itafanyika huko nchi Brazil.

Jamieson mwenye umri wa miaka 28 alitwaa medali ya fedha wa katika michuano ya olimpic iliyopita.

Muogeleaji huyu alishika nafasi ya tano katika mbio za majaribio za mita 200 katika michezo iliyofanyika mjini Glasgow siku ya ijumaa huku wanaufuzu ni wawili wa nafasi za juu.

Jamieson amekua na miaka miwili migumu ikiwa ni pamoja nakusumbuliwa na moyo na kupoteza mchezo dhidi ya mpinzani Ross Murdoch katika michuano ya jumuia ya madola.