Fa kumuadhibu Vardy

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Jamie Vardy

Mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy amefunguliwa mashtaka ya utovu wa nidhamu na chama cha soka cha nchini England FA.

Vardy alifanya vitendo vya utovu wa nidhamu baada ya kupewa kadi nyekundu na mwamuzi Jon Moss katika mchezo wa Jumapili dhidi ya West Ham.

Ripoti ya mwamuzi huyo imedai kuwa mshambuliaji huyo alifanya utovu wa nidhamu kwa majibu yake mara baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu na ndio maana amefunguliwa mashtaka hayo.

Iwapo atapatikana na hatia, bali ya kuzuiwa kucheza mechi 1 kutokana cha kadi nyekundu sasa anaweza kufungiwa zaidi ya hapo. FA pia imefungulia mashtaka Leicester City kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wao wakati wa mechi hiyo hiyo na West Ham.