Barcelona yaiua Deportivo

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Lionel Messi

Klabu ya soka ya Barcelona imepata ushindi wa kishindo kwa kuichapa Deportivo La Coruna mabao 8-0. Mshambuliji wa Luis Suarez akianza kufunga bao la kwanza dakika ya 11 kisha akaongeza mengine matatu katika dakika ya 24' 53' 64 . Mabao mengine ya timu hiyo yalifungwa na kiungo Ivan Ivan Rakitic, beki Marc Bartra na nyota wa wawili wa timu hiyo lionel Messi na Neymer jr wakifunga bao moja moja kila mmoja.

Barcelona wanaendelea kuongoza ligi wakiwa na alama 79 wakifuatiwa na Atletico Madridi wenye alama 79 pia ila wakipishana kwa idadi ya magoli ya kufunga huku Real Madrid wakiwa nafasi ya tatu kwa alama 78.