Arsenal kuchuana na West Bromwich

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Arsene Wenger

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger atakifanyia mabadiliko kikosi chake kufuatia sare ya 1-1 dhidi ya kilabu ya Crystal Palace wikendi iliopita.

Per Mertesacker,Aaron Ramsey ,Theo Walcot na Olivier Giroud huenda wakaanzishwa lakini Jack Wilshere hayuko tayari kucheza.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wachezaji wa Arsenal

Upande wa timu ya West Brom, hakuna majeraha yotote yalioripotiwa tangu washindwe na Watford.

Saido Berahino anatarajiwa kuanza katika safu ya mashambulizi licha ya kukosa mikwaju miwili ya penalti dhidi ya Hornets,Alex Pritchard huenda asicheze,huku James Morrison akiwa hatocheza.