Arsenal yaichabanga West Brom

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Alexis Sanchez

Washika bunduki wa London Arsenal wakicheza katika uwanja wao wa Emirate wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya West Bromwich Albion.

Mshambuliaji Alexis Sanchez ndie alikuwa shujaa wa mchezo huo baada ya kuzipasia nyavu mara mbili alianza kufunga goli la kwa katika dakika ya 6 ya mchezo kisha akifunga goli la pili kwa mpira wa adhabu katika dakika ya 38.

Katika mchezo huo timu ya Arsenal iliutawala kwa asilimia 71, huku West Brom wakiutawala kwa asilimia 29. Kwa ushindi huo vijana wa Profesa Arsenal Wenger, wanajiweka katika nafasi nzuri ya kuwa kwenye nne bora baada ya kujikusanyia alama 63 katika michezo 34 waliyocheza.

Arsenal wamesaliwa na michezo minne mkono kabla ya kumalizika kwa ligi kuu England msimu