Kikosi bora cha mwaka cha PFA

Haki miliki ya picha Getty

Timu za Leicester City na Tottenham imetoa wachezaji wanane katika kikosi cha mwaka cha wachezaji bora wa wa kulipiwa (PFA) wa Ligi Kuu ya England.

Kila timu ikiwa imetoa wachezaji wanne wa kikosi hicho bora cha msimu huu.

Washambuliaji Jamie Vardy na Harry Kane kuu ndio wanaongoza safu ya mashambulizi ya kikosi hicho.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mesut Ozil

Kiungo wa Kijerumani Mesut Ozil ambaye anawania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa chama cha wanasoka wa kulipwa PFA hayumo kwenye kikosi hicho.

PFA walikuwa wakitangaze kikosi hicho siku ya Jumapili ijayo katika sherehe za utoaji tuzo lakini kwa sababu ya siri za kikosi kuvuja ikawabidi chama hicho kutangaza mapema kabla ya siku waliyopanga.

Kikosi kamili: