Ranieri: Lazima tushinde ligi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Claudio Ranieri

Mkufunzi wa kilabu ya Leicester Claudio Ranieri anaamini kwamba ni kazi ya kufa na kupona kwa kilabu yake kushinda ligi ya Uingereza.

Viongozi hao wa ligi wamekuwa na kampeni nzuri ya kushinda taji hilo na sasa wako pointi tano juu ya kilabu ya Tottenham ikiwa zimesalia mechi nne.

Siku ya Jumapili wataikaribisha nyumbani Swansea.

Kufikia sasa kilabu hiyo ina hakika ya kushiriki katika mechi za kilabu bingwa Ulaya baada ya kujihakikishia kumaliza katika timu tatu bora, na Ranieri anasema kuwa lengo lake kuu sasa ni kushinda taji la ligi.''Ni mwaka huu ama isifanyike tena''.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ranieri

''Tumefanikiwa kufuzu katika michuano ya kombe la vilabu bingwa,ni ufanisi mkubwa kwa kila mtu lakini sasa tunajaribu kushinda taji la ligi na nguvu zetu zote.

Nimewaambia wachezaji wangu kwamba sasa ndio wakati mzuri wa kuweka nguvu zote.Tunahitaji pointi nane tushinde taji.Na tutajaribu kufanya hivyo